Wednesday, December 19, 2012

HISTORIA YA MKOA WA MTWARA

 Na Cosmas Pahala
Masasi


1. UTANGULIZI
1.1 HISTORIA FUPI YA MKOA WA MTWARA
Mfumo wa utawala wa ukoloni uliigawa Tanzania katika Majimbo 8, Mkoa wa Mtwara
ulikuwa ndani ya Jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara
ambapo Makao Makuu ya Jimbo yalikuwa Lindi.

Mkoa wa Mtwara ulianzishwa rasmi mwaka 1971 kutokana na Mpango wa Madaraka Mikoani
ambao ulilenga kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Mkoa huu ulipoanzishwa ulikuwa tayari na Wilaya tatu (3) ambazo ni Masasi iliyoanzishwa
mwaka 1928 chini ya ukoloni wa Kijerumani, Newala mwaka 1956 chini ya wakoloni wa
Kiingereza na Mtwara ilianzishwa mwaka 1961.


 Kutokana na ongezeko la watu na kukua kwa
Mkoa wa Mtwara ziliongezeka Wilaya nyingine 2 ambazo ni Wilaya ya Tandahimba
iliyoanzishwa mwaka 1995 kutoka kwenye Wilaya ya Newala na Nanyumbu ilianzishwa
mwaka 2006 kutoka Wilaya ya Masasi.
Kiutawala Mkoa umegawanyika katika Wilaya 5 na Halmashauri 6, Tarafa 25, Kata 149, Vijiji
738, Vitongoji 3,126 na Mitaa 85. Aidha, Mkoa unatarajia kuwa na Halmashauri ya Mji wa
Masasi.
2
Mchoro Na.1: Ramani ya Mkoa wa Mtwara.
Takwimu za kiutawala ni kama zinavyoonekana katika jedwali hapa chini.
Jedwali Na.1: Takwimu za Kiutawala Mkoa wa Mtwara
1.2 MAANA YA NENO MTWARA
Neno Mtwara limetokana na neno la lugha ya Kimakonde “kutwala” ikiwa na maana ya
kuchukua (kunyakua) kitu chochote.
Mtwara ni Jina inalotumika kwa maana 3 tofuati zifuatazo:
• Mtwara jina la Mkoa.
• Mtwara jina la mji wa Makao Makuu ya Mkoa.
• Mtwara ni Wilaya na Makao Makuu ya Wilaya ambayo kiutawala ina Halmashauri 2,
ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Halmashauri ya Mtwara.
Na. Halmashauri Tarafa Kata Vijiji Mitaa Vitongoji Idadi ya
watu
1 MTWARA MIKINDANI 2 15 6 85 27 126,923
2 MTWARA 6 28 157 0 638 234,563
3 MASASI 5 34 174 0 905 374,139
4 NEWALA 5 28 155 0 471 214,766
5 NANYUMBU 4 14 89 0 504 154,960
6 TANDAHIMBA 3 30 157 0 581 243,885
JUMLA 25 149 738 85 3126 1,349,236
3
Mkoa wa Mtwara una makabila makuu 3 ambayo ni Wamakonde wanaopatikana katika
Wilaya za Mtwara, Tandahimba na Newala, Wayao na Wamakua wanaopatikana katika
Wilaya za Masasi na Nanyumbu. Kihistoria makabila haya, hapo awali yaliishi pamoja na
makabila mengine kaskazini mwa mto Ruvuma. Makabila hayo yaliacha makazi yao na
kukimbilia Msumbiji kutokana na uvamizi na vita vya makabila kutoka kaskazini mwa
Tanganyika. Katika kuishi Msumbiji matarajio yao ya kuishi kwa amani na utulivu
yalitoweka kutokana na kuibuka kwa vita vya Wazulu. Vita hivyo vilisababisha makabila
hayo kurudi ng’ambo ya mto Ruvuma yalikokuwa zamani. Baada ya kuvuka mto Ruvuma,
Wamakonde, Wayao na Wamakua walitafuta maficho hadi kufikia katika bonde la
Mkatahumbo na Chitandi. Walitulia katika maeneo hayo na kuondokana na wasiwasi wa
kukamatwa na Wazulu.
1.3 MAHALI MKOA ULIPO
Mkoa huu upo Kusini kabisa mwa Tanzania. Kijiografia upo kati ya Longitudo 38° na 40°
Mashariki ya Griniwichi, na kati ya Latitudo 10° 05”na 11° 25” kusini ya Ikweta, na una eneo
la Kilomita za mraba 16,720 ambayo ni sawa na asilimia 1.9 (1.9%) ya eneo la Tanzania Bara
ambalo ni kilomita za mraba 885,987. Takribani asilimia 3.91 (hkt 65,450) ya eneo la Mkoa
lipo chini ya hifadhi mbili za wanyama ambazo ni Msanjesi (hkt 44,425) na
Lukwika/Lumesule (hkt 21,025).
Mkoa wa Mtwara kwa upande wa Kaskazini umepakana na Mkoa wa Lindi, upande wa
Mashariki umepakana na Bahari ya Hindi, upande wa Kusini kuna Mto Ruvuma
unaotenganisha Tanzania na Msumbiji, wakati upande wa Magharibi umepakana na Mkoa wa
Ruvuma.
4
1.4 HALI YA HEWA
Mkoa wa Mtwara una vipindi viwili vikuu vya majira. Majira ya mvua ambayo huitwa
MASIKA na majira ya ukavu ambayo huitwa KIANGAZI. Hakuna mvua za msimu maalum
kama vile za Vuli zinazopatikana sehemu nyingine Tanzania. Kwa kawaida Mkoa wa Mtwara
hupata mvua ya wastani wa mm 935 hadi 1,166 kwa mwaka. Wilaya inayoongoza kupata
mvua nyingi ni Newala ambayo hupata wastani wa mm.1001, Wilaya inayopata mvua kidogo
ni Nanyumbu ambayo hupata wastani wa mm.832.
Kwa kawaida kiwango cha juu cha joto Mkoani Mtwara ni 32C mwezi Disemba na kiwango
cha chini cha joto huwa ni 28C mwezi Julai.
1.5 AINA YA UDONGO
Udongo hutegemea hali ya jiolojia. Katika Mkoa huu kuna kanda mbili za kijiolojia. Kwanza
ni ukanda wa pwani ambao unaendelea kwa kilomita 125 kutoka bahari ya Hindi hadi ukanda
wa Makonde uliopo Newala. Ukanda huu udongo wake ni wa kichanga na wenye rutuba hafifu
na uwezo mdogo wa kushikilia maji. Maeneo mengine katika ukanda huu yana udongo mzito
wa aina ya mfinyanzi. Vilevile mawe ya chokaaa yaliyopo pwani hutoa udongo mwekundu
unaopitisha maji vizuri.
Ukanda wa pili wa kijioliojia huendelea Magharibi ya ukanda wa pwani, ukanda huu una asili
ya mawe yaliojishindilia kwa chini. Kaskazini ya mji wa Masasi kuna udongo wa mfinyanzi
uliochangayika na udongo mwekundu, udongo huu ndio bora kuliko aina zote kwani ndio
unaofaa kwa mazao ya chakula na biashara.
5
1.6 WAKAZI WA MKOA WA MTWARA NA SHUGHULI ZAO.
Shughuli kubwa ya kiuchumi Mkoani Mtwara ni kilimo, ambapo inakadiriwa kuwa 92% ya
wakazi wa Mtwara wanajishughulisha na kilimo. Shughuli nyingine muhimu ni uvuvi, ufugaji
wa nyuki na viwanda vidogo vidogo. Karibu 85% ya eneo la Mkoa wa Mtwara linafaa kwa
kilimo, hata hivyo eneo linalotumika kwa shughuli za kilimo ni chini ya 20%. Jembe la mkono
ndio zana kubwa inayotumika katika shughuli za kilimo Mkoani Mtwara, hata hivyo serikali
inafanya juhudi kuwawezesha wananchi kutumia zana bora za kilimo kama matrekta makubwa
na madogo.
2. MUUNDO WA MKOA WA MTWARA ULIVYOBADILIKA KATIKA NYAKATI
TOFAUTI KUANZIA 1961
Baada ya uhuru Mkoa wa Mtwara uliendelea kuwa ni sehemu ya Jimbo la Kusini. Jimbo la
Kusini wakati huo lilijumuisha Ruvuma, Lindi na Mtwara likiwa na Wilaya 9 ambazo ni
Newala, Masasi, Mtwara, Nachingwea, Lindi, Kilwa, Tunduru, Songea na Mbinga. Kiongozi
wa Jimbo alijulikana kama Gavana.
Katika kuhakikisha kuwa huduma za jamii zinasogezwa karibu na wananchi, mwaka 1962
Serikali ilivunja Jimbo la Kusini na kuanzisha Mikoa miwili ya Ruvuma na Mtwara. Mkoa wa
Mtwara ulijumuisha eneo la Lindi na Mtwara na Makao yake Makuu yalikuwa Mtwara. Kwa
dhamira ile ile ya kusogeza huduma karibu na wananchi, mwaka 1971 Serikali iliamua
kugawanya Mkoa wa Mtwara na kuwa na Mikoa ya Lindi na Mtwara.
6
Katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuwapa wananchi madaraka ya kuamua mambo
yanayohusu maendeleo yao, mwaka 1971 iliamua kuanzisha mpango wa Madaraka Mikoani.
Muundo huo uliendelea hadi kufikia mwaka 1982 ilipoanzisha Serikali za Mitaa na hatimaye
mwaka 1997 Serikali ilitunga Sheria Na. 19 iliyounda Sekretarieti za Mikoa zilizoanza rasmi
mwaka 1999.
3. MAJUKUMU NA MALENGO YA MKOA WA MTWARA
Dira ya Mkoa ni kuzijengea uwezo serikali za mitaa ili kuziwezesha kujiendesha kwa misingi
ya Utawala Bora na kutoa huduma bora kwa wananchi ili kujiletea maendeleo endelevu ya
kijamii na kiuchumi kwa kushirikiana na wadau wengine. Katika kufikia azma hii Mkoa
umejielekeza kutekeleza majukumu yafuatayo;
1. Kutekeleza miradi inayolenga katika kupunguza umaskini hususani miradi ya elimu, afya,
maji, barabara na kilimo.
2. Kufuatilia na kuhakikisha kwamba mipango ya maendeleo ya Mkoa na Halmashauri
inatekelezwa kwa ukamilifu na malengo yake yanafanikiwa.
3. Kuhakikisha kwamba kunakuwepo na utekelezaji wa sera za kisekta na programu za
maendeleo katika Halmashauri.
4. Kuhakikisha kwamba kunakuwepo na utekelezaji wa sera zinazolenga katika kupambana
na Ukimwi, vita dhidi ya rushwa, uharibifu wa mazingira na utekelezaji wa maagizo ya
Serikali kuu kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
5. Kufuatilia na kuhakikisha kwamba kero za wananchi zinaondolewa kwa kufuata sheria,
kanuni, taratibu na haki.
7
4. HALI YA UONGOZI NA UTAWALA KUANZIA 1961
Kabla ya uhuru, miaka ya mwisho ya ukoloni Wilaya zilikuwa chini ya Mamlaka ya
Halmashauri iliyojulikana kama “Native Authority”. Baada ya uhuru mfumo wa utawala
ulibadilika na kuwa wa Serikali za Mitaa. Katika kipindi cha mwaka 1971-1980 mfumo wa
utawala ulibadilika tena na kuwa wa Madaraka Mikoani ukijumuisha Wakuu wa Mikoa ambao
walifahamika kama ”Regional Commissioner”, Wakuu wa Wilaya ambao walijulikana kama
”Area Commissioners”, Afisa Tawala Wilaya au ”District Administrative Officer”, Makatibu
Tarafa na Makatibu Kata.
Kiutendaji katika ngazi ya Mkoa kulikuwa na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa (Regional
Development Director) na Wakuu wa Idara wa Kisekta. Katika ngazi ya Wilaya Mtendaji
Mkuu alikuwa ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya (District Development Director)
akisaidiwa na Wakuu wa Idara wa Kisekta.
Muundo huo uliendelea hadi kufika mwaka 1997 ambapo ulibadilishwa kupitia Sheria Na. 19
iliyounda rasmi Sekretarieti za Mikoa na kubadilisha muundo wa utawala kama ifuatavyo:
8
Mchoro Na. 2: Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwaka 2007.
Kuanzia mwaka 1961 hadi 2011 Mkoa wa Mtwara uliongozwa na Wakuu wa Mkoa wafuatao:-
Mkuu wa Mkoa
Katibu Tawala Mkoa
Hospitali ya Mkoa
Mganga Mfawidhi
Mkuu wa Wilaya
Katibu Tawala Wilaya
Katibu Tarafa
Mamlaka ya Serikali za Mitaa Kikao cha Ushauri wa Wilaya
Seksheni ya
Utawala na
Rasilimali Watu
Katibu Tawala
Msaidizi
Kitengo cha
Uhasibu
Mhasibu Mkoa
Mkaguzi wa
Ndani
Mkaguzi wa
Ndani Mkoa
Kitengo cha
Manunuzi
Afisa Ugavi Mkuu
Seksheni ya
Huduma za Jamii
Katibu Tawala
Msaidizi
Seksheni ya
Uchumi na
Uzalishaji
Katibu Tawala
Msaidizi
Seksheni ya
Miundombinu
Katibu Tawala
Msaidizi
Seksheni ya
Menejimenti
ya Serikali za
Mitaa
Katibu Tawala
Msaidizi
Seksheni ya
Mipango na
Uratibu
Katibu Tawala
Msaidizi
Kikao cha Ushauri wa
Mkoa
9
Jedwali Na. 2: Orodha ya Wakuu wa Mkoa wa Mtwara
Na Jina Kipindi/Mwaka
1 Bw. John Nzunda 1962-1972
2 Dr.Wilbert Kleruu 1972-1974
3 Balozi Charles Kileo 1974-1977
4 Lt. Col Kabenga Nsa Kaisi 1978-1980
5 Bw.Lawi Nangwanda
Sijaona
1980-1981
6 Bw. Ibrahim Sufian
Kajembo
1981-Desemba 1990
7 Col. Ferdinand Swai Desemba 1990-Februari
1992
8 Bibi Kate Kamba Februari 1992-Mei 1994
9 Col. Kabenga Nsa Kaisi Mei 1994-Februari 2003
10 Bw. Isidore Leka Shirima Februari 2003-Januari 2006
11 Bw.Henry Daffa Shekifu Februari 2006-Aprili 2007
12 Col.Mst. Anatoli A Tarimo Mei 2006-hadi sasa
5. SERA NA SHERIA ZILIZOKUWEPO TANGU UHURU KATIKA MFUMO WA
KISIASA, KIULINZI, KIUTAWALA, KIUCHUMI, KITEKNOLOJIA NA KIJAMII
Mkoa wa Mtwara kama ilivyo Mikoa mingine ya Tanzania ilifuata na kutekeleza sera na sheria
mbalimbali zilizotungwa na Taifa, Sera hizo ni pamoja na:-
5.1 KISIASA
• Baada ya uhuru siasa iliyokuwepo ni ya ubepari na kulikuwa na mfumo wa vyama
vingi vya siasa hadi mwaka 1965 ulipoanzishwa mfumo wa chama kimoja cha Siasa
ambacho kilikuwa TANU (Tanganyika African National Union).
• Mwaka 1967 mfumo wa Siasa ya kibepari ulibadilishwa kutokana na kutangazwa kwa
Azimio la Arusha ambalo lilianzisha mfumo wa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
10
• Mwaka 1992 ulianzishwa mfumo wa vyama vingi vya Siasa, ambapo kwa sasa Mkoa
wa Mtwara una vyama 12 vya siasa vifuatavyo:-
􀀹 Chama Cha Mapinduzi (CCM)
􀀹 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
􀀹 Chama cha Wananchi (CUF)
􀀹 Tanzania Labour Party (TLP)
􀀹 United Democratic Party (UDP)
􀀹 APPT Maendeleo
􀀹 SAU
􀀹 NCCR-Mageuzi
􀀹 NLD
􀀹 Democratic Party (DP)
􀀹 TADEA
􀀹 UPDP
5.2 KIULINZI
Kiulinzi Mkoa wa Mtwara umetekeleza sera mbalimbali za kiulinzi ambapo Jeshi lililokuwa
linaendelea na ulinzi mara baada ya Tanganyika kupata uhuru ni Jeshi la Mfalme wa Uingereza
lililojulikana kama (King African Rifle). Jeshi hili liliendelea na kazi ya ulinzi hadi mwaka
1964 lilipoanzishwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) chini ya Amiri Jeshi Mkuu Rais
wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Majeshi mengine yaliyokuwepo ni pamoja na Jeshi la Polisi kwa ajili ya usalama wa raia na
11
mali zao, Jeshi la Magereza kwa ajili ya kurekebisha tabia za waharifu, Jeshi la Mgambo kama
wasaidizi wa ulinzi wa raia na Ulinzi wa jadi.
Aidha, kutokana na harakati za kudai uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika kama vile
Msumbiji, Angola, Zimbabwe na Afrika Kusini. Mkoa wa Mtwara ulikuwa moja kati ya vituo
vya mapambano ya ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.
5.3 KIUTAWALA
Wakati wa uhuru Mkoa ulikuwa na wilaya tatu ambazo ni Masasi, Newala na Mtwara, baadaye
Wilaya nyingine mbili ambazo ni Tandahimba 1995 na Nanyumbu 2006 zilianzishwa.
5.4 KIUCHUMI
Kuanzia mwaka 1967 hadi 1991 mfumo wa uchumi wa Taifa ulikuwa ni hodhi ambapo bei za
bidhaa zilipangwa na kusimamiwa na Serikali. Aidha, njia kuu za uchumi zilimilikiwa na
Umma. Mwaka 1992 mfumo huu wa uchumi ulibadilika kuwa mfumo wa soko huria na sera ya
ubinafsishaji ilianzishwa na kutekelezwa.
5.5 KITEKNOLOJIA
Baada ya uhuru teknolojia habari na mawasiliano iliyokuwa inatumika ilikuwa ni ya Analojia
na baadaye tuliingia kwenye mfumo wa digitali.
5.6 KIJAMII
12
Mara baada ya uhuru wananchi waliendelea kuishi kwenye maeneo yao ya asili na mfumo wa
mahusiano na Utawala uliongozwa na viongozi wa Kimila. Mkoa wa Mtwara ni kati ya Mikoa
ya mwanzo iliyotekeleza kikamilifu Sera ya vijiji ya mwaka 1973 na hatimaye Sera ya vijiji
vya Ujamaa ya mwaka 1974. Mnamo mwaka 1975 wananchi wote katika maeneo ya vijijini
walikuwa wanaishi katika vijiji vya Ujamaa.
6. MABADILIKO NA MATUKIO MAKUU
6.1 MABADILIKO
6.1.1. KISIASA
Tangu ulipoanza mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, chaguzi zote zilizofanyika
mwaka 1995 na 2000 nafasi zote za uongozi zilichukuliwa na chama Tawala (Chama Cha
Mapinduzi). Katika uchaguzi wa 2000 chama cha TLP kilishinda kiti kimoja cha udiwani
Wilaya ya Masasi na 2010 baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani vimeweza kupata ushindi
wa viti vya vijiji na Udiwani, Chama kinachoongoza kwa upinzani ni Chama cha Wananchi
(CUF).
Jedwali lifuatalo linaonyesha matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010 viti vya Udiwani Mkoani
Mtwara.
Jedwali namba 3: Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Udiwani Mkoa
wa Mtwara mwaka 2010
Jimbo Idadi
ya
kata
Chama Ushindi wa
Udiwani kwa
Kata
Asilimia
Lulindi 15 CCM 15 100
Masasi 19 CCM 19 100
Nanyumbu 14 CCM
CUF
CHADEMA
12
I
1
85
7.5
7.5
13
Newala 28 CCM 28 100
Tandahimba 30 CCM
CUF
21
9
70
30
Mtwara
Vijijini
28 CCM
CUF
26
2
93
7
Mtwara
Mjini
15 CCM 15 100
6.1.2 KIUCHUMI
6.1.2.1 Kilimo
Shughuli kubwa ya kiuchumi kwa Mkoa wa Mtwara ni kilimo, asilimia 85 ya eneo la Mkoa
linafaa kwa kilimo. Uzoefu unaonesha kuwa sehemu kubwa ya wakazi wa Mtwara
wanajihusisha na kilimo, ambapo asilimia 86.4 ya wakazi wake hujishughulisha na kilimo cha
mazao ya biashara na chakula ambayo ni Korosho, Minazi, Muhogo, Ufuta, Mtama, Mbaazi,
Karanga, Mpunga, Choroko, Kunde na Mahindi.
Mkoa umeendelea kufanya jitihada zinazolenga kuhakikisha kwamba wananchi wake
wanatumia fursa zilizopo Mkoani, kwa maana ya Ardhi nzuri na yenye rutuba, Hali nzuri ya
hewa, Miundombinu ya Barabara na Bandari, Nishati ya gesi na umeme na Uwekezaji ili
kujiletea maendeleo kupitia Kilimo cha Mazao mbalimbali ya chakula na biashara, Ufugaji,
Ushirika, Maliasili na Uvuvi.
Katika kuhakikisha kuwa kilimo kinaleta tija kwa wananchi na hivyo kuwaletea maendeleo,
Mkoa umeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kilimo inayowezesha kuleta mabadiliko
ya haraka katika maisha ya wakulima kupitia Sekta ya Kilimo. Mikakati hii imepangwa na
inatekelezwa na kila Wilaya kupitia Programu ya Maendeleo ya Kilimo inayojulikana kama
ASDP kitaifa au DADPs kwa ngazi za Wilaya.
14
Maeneo makuu yaliyoainishwa na kupewa kipaumbele ili kuleta mapinduzi hayo ni pamoja na
Uimarishaji wa huduma za Ugani, Matumizi ya Zana bora za Kilimo, Uendelezaji wa Kilimo
cha Umwagiliaji, Matumizi ya Pembejeo bora za kilimo, Usindikaji wa Mazao ya Kilimo,
Uimarishaji wa Ushirika na Masoko ya mazao na Ushirika wa Kuweka na Kukopa.
• Uimarishaji wa Huduma za Ugani Mkoani.
Mkoa kwa kushirikiana na Wilaya zake unatekeleza Mfumo wa utoaji huduma za ugani kwa
wakulima kupitia Mashamba Darasa ngazi za Vitongoji. Utaratibu huu umewawezesha
wakulima ambao kwa muda mrefu hawakupata fursa ya kukutana na Wataalam wa kilimo,
kupata fursa hiyo na kujifunza mbinu sahihi za kilimo bora kwa vitendo.
Picha Na:1 Shamba Darasa La Mihogo Kitongoji Cha Namichi Wilayani Masasi.
Mashamba darasa yameongezeka kutoka 375 msimu wa 2008/2009 na kuwa 3,105 msimu wa
2010/2011, kwa mchanganuo ufuatao:
15
Jedwali Na. 4: Idadi ya Mashamba Darasa kwa kila Halmashauri Mwaka 2008/2009,
2009/2010 na 2010/2011
Halmashauri
Idadi ya
Vitongoji
Idadi ya Vitongoji
vyenye mashamba
darasa 2008/2009
Idadi ya
mashamba
darasa 2009/2010
Idadi ya
mashamba
darasa
2010/2011
Mtwara/Mikindani 35 6 27 35
Mtwara 638 52 618 618
Newala 466 136 466 466
Masasi 905 120 905 893
Tandahimba 589 7 581 589
Nanyumbu 504 54 488 504
Jumla 3,137 375 3,085 3,105
• Huduma kwa Bwana Shamba/Bibi Shamba kwa Mwaka 2010/2011
Moja kati ya matatizo yaliyofanya kilimo kukosa tija katika Mkoa wa Mtwara mara baada ya
Uhuru ni uhaba wa Maafisa Ugani na vitendea kazi kwa Maafisa hao na hivyo kufanya
wakulima kutoweza kupata ushauri wa kitaalamu wa kilimo. Mpaka kufikia mwaka 2011
Mkoa wa Mtwara una jumla ya Maafisa Ugani 69 na wote wamepatiwa pikipiki ili kuwafikia
wakulima kwa urahisi.
• Matumizi ya Teknolojia bora za Kilimo.
Baada ya uhuru zana zilizokuwa zinatumika ni majembe madogo maarufu kwa jina la
Chingondola au Mgwilili, Panga na Mundu. Matumizi ya Maksai yalianza mwaka 1980 kwa
majaribio katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Newala. Kuanzia mwaka 1983
matrekta makubwa yalianza kutumika ambapo ekari moja ililimwa kwa shilingi 45.
Kwa sasa Mkoa unalenga kuongeza matumizi ya zana za kisasa katika kilimo kama matrekta
makubwa na madogo ya kusukuma kwa mkono (Power Tillers). Katika kutekeleza azma hii,
mwaka 2008/2009 hadi 2010/2011 jumla ya matrekta makubwa 66 na madogo 228

DOGO RK, AIBUKA KINARA KATIKA TAMASHA LA VIPAJI HALISI


 Na Cosmas Pahalah
Masasi

Tamasha la kusaka na kuibua vipaji vya uimbaji wa muziki wa kizazi kipya (SHANGWE ZA VIPAJI HALISI) lililo andaliwa na Pax media production kwa hisani ya Masasi house of wine na stadom school of journalism, limefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa mikutano wa Mtavala uliopo mjini masasi, ambapo mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Afsa utamaduni wa wilaya ya masasi nd
ugu Abdul Milanzi.

Aidha washindi watatu katika tamasha hilo waepata furusa ya kusaini lebo na Pax media, mshiriki anaye julikana kama Razaki Adamu maarufu kama DOGO RK  (miaka 13) aliibuka kuwa kinara wa muziki wa kizazi kipya mjini Masasi, washindi wengine ni pamoja na Hamza Macheche (Cheche boy) na Hamisi Mohamed (Jojo).

Akizungumza katika tamasha hilo mkurugenzi wa Pax media, bwana Innocent Aloyce alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni Kutambulisha wasanii na kazi zao kwa umma wa Masasi ili waweze kutambulika na kutumika kama mabalozi wa shughuli mbalimbali za kiserikali na za kijamii, na Kutafuta wasanii wakudumu watakaofanya kazi chini ya uangalizi wa Pax media.
  
Pia bwana Innocent Aloyce aliongeza kwa kusema kuwa ameamua kujishughulisha na shughuli za kuibua na kukuza vipaji vya uimbaji katika mji wa masasi kutokana kukerwwa na tabia ya watu wa wilaya ya masasi ya kutothamini vijana wao hususani wanaofanya muziki wa kizazi kipya kwa dhana ya kuwa muziki ni uhuni.
 
“Wakati watu kusini tukiwa na dhana iliyopitwa na wakati ya kuwa muziki wa kizazi kipya ni uhuni, wenzetu waliopiga hatua katika masualaya muziki na burudani wanautukuza usemi usemao mcheza kwao hutuzwa na kuutupilia mbali msemo wa Nabii hakubaliki kwao”.

Pia bwana Inocent aliongeza kwa kusema, Pax media inaunga mkono msemo wa kimakua usemao ERRIYE AFYANA VATENDA VANI? Yaani tusipo jivunia vya nyumbani tutajivunia nini?

Pia mkuu wa chuo cha uandishi wa habari cha STADOM, bwana Edwin Ekon aliwazawadia washindi watatu nafasi ya masomo (schoolaship) ya kusomea uandishi wa habari bure katika chuo cha stadom.
Bw. Ekon aliwataka pia washiriki wa shindano la uimbaji katika tamasha hilo kurekodi nyimbo ya pamoja (audio na video) ambayo itagharamiwa na Stadom school of journalism.