Na Cosmas Pahalah
Masasi
Tamasha la kusaka na kuibua vipaji vya uimbaji wa muziki wa kizazi kipya (SHANGWE ZA VIPAJI HALISI) lililo andaliwa na Pax media production kwa hisani ya Masasi house of wine na stadom school of journalism, limefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa mikutano wa Mtavala uliopo mjini masasi, ambapo mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Afsa utamaduni wa wilaya ya masasi nd
Masasi
Tamasha la kusaka na kuibua vipaji vya uimbaji wa muziki wa kizazi kipya (SHANGWE ZA VIPAJI HALISI) lililo andaliwa na Pax media production kwa hisani ya Masasi house of wine na stadom school of journalism, limefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa mikutano wa Mtavala uliopo mjini masasi, ambapo mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Afsa utamaduni wa wilaya ya masasi nd
ugu Abdul Milanzi.
Aidha washindi
watatu katika tamasha hilo waepata furusa ya kusaini lebo na Pax media, mshiriki
anaye julikana kama Razaki Adamu maarufu kama DOGO RK (miaka 13) aliibuka kuwa kinara wa muziki wa
kizazi kipya mjini Masasi, washindi wengine ni pamoja na Hamza Macheche (Cheche
boy) na Hamisi Mohamed (Jojo).
Akizungumza katika
tamasha hilo mkurugenzi wa Pax media, bwana Innocent Aloyce alisema kuwa lengo
la tamasha hilo ni Kutambulisha wasanii na kazi zao kwa umma wa Masasi ili
waweze kutambulika na kutumika kama mabalozi wa shughuli mbalimbali za kiserikali
na za kijamii, na Kutafuta wasanii wakudumu watakaofanya kazi chini ya
uangalizi wa Pax media.
Pia bwana Innocent Aloyce aliongeza kwa kusema kuwa ameamua
kujishughulisha na shughuli za kuibua na kukuza vipaji vya uimbaji katika mji
wa masasi kutokana kukerwwa na tabia ya watu wa wilaya ya masasi ya kutothamini
vijana wao hususani wanaofanya muziki wa kizazi kipya kwa dhana ya kuwa muziki
ni uhuni.
“Wakati watu kusini tukiwa na dhana iliyopitwa
na wakati ya kuwa muziki wa kizazi kipya ni uhuni, wenzetu waliopiga hatua
katika masualaya muziki na burudani wanautukuza usemi usemao mcheza kwao
hutuzwa na kuutupilia mbali msemo wa Nabii hakubaliki kwao”.
Pia bwana Inocent aliongeza kwa
kusema, Pax media inaunga mkono msemo wa kimakua usemao ERRIYE AFYANA VATENDA VANI? Yaani tusipo jivunia vya nyumbani
tutajivunia nini?
Pia mkuu wa chuo cha uandishi wa
habari cha STADOM, bwana Edwin Ekon aliwazawadia washindi watatu nafasi ya
masomo (schoolaship) ya kusomea uandishi wa habari bure katika chuo cha stadom.
Bw. Ekon aliwataka pia washiriki wa
shindano la uimbaji katika tamasha hilo kurekodi nyimbo ya pamoja (audio na
video) ambayo itagharamiwa na Stadom school of journalism.
No comments:
Post a Comment